Mitazamo Ya T.I kuhusu Muziki Wa Nicki Minaj Na Cardi B
Wiki iliyopita T.I aliingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuachia majina ya wanamuziki hamsini wa Hip Hop anaowakubali muda wote.
Kwenye Top 50 yake T.I amemuandika Tupac kwenye nafasi ya kwanza huku list hiyo ikipambwa na majina mengine kama Jay-Z, Eminem, Nelly, Future, Gucci na Nicki Minaj ambaye alimuandika kwenye namba kati ya 41 na 42.
Mashabiki wakapenda kujua vipi kuhusu Cardi B ambaye hakuwepo kwenye list hiyo ingawa anafanya muziki mkubwa na ameendelea kuvunja rekodi nyingi za wanamuziki wa kike.
T.I amesema hakufikiria kama majina ya Nicki na Cardi yalistahili kuwepo kwenye list hiyo kwa pamoja ikiwa wote wawili wanafanya kitu kimoja, kauli ambayo iliwachefua mashabiki wa Nicki Minaj waliomkosoa T.I kwa kumwambia Cardi B ni rappa anayefanya muziki wa ovyo usiofanana kabisa na ule wa Nicki Minaj.
Kwenye mahojiano na Rap Radar, T.I alikutanishwa na Cardi B kuzungumzia mashindano ya Rythm & Flow ambapo wote wawili ni majaji, pamoja hiyo pia aliongelea maoni yake ambapo aliwacharukia wote waliomkosoa kwa kumlazimisha asimamie upande mmoja linapokuja suala la kuwaunga mkono wanamuziki wa kike.
TIP amesema yeye ana mitazamo yake na uhuru wa kufikiria anachokitaka, Mkali huyo wa ngoma ya ‘sabotage’ amewataja Nicki Minaj na Cardi B kama wasichana ambao wamekuwa na historia nzuri kwenye muziki wao, wametokea mbali na wote wana mafanikio ya kuigwa hivyo wana kila sababu ya kuendelea kupewa nafasi.
3,464 total views, 3 views today