MSANII na mwigizaji, Lauren London, amepata kibali cha kusimamia fedha ya urithi kwa mwanaye wa kiume, Kross, aliyezaa na mwanamuziki Nipsey.Mambo hayajawa rahisi pia kwa Tanisha Foster, ambaye naye alizaa na Nipsey binti aitwaye Emani akiwa sasa ana umri wa miaka 10. Binti huyo naye yumo katika mgao wa urith wa Nipsey, lakini pamekuwa hapana uelewano baina ya kaka na dada yake Nipsey.Nipsey aliuawa nje ya duka lake huko Los Angeles mwaka huu.Eric Holder, mtuhumiwa aliyemuua Nipsey, hivi sasa anakabiliwa na makosa ya kuua na kuwa bastola isivyo halali.