Sambaza

Mwarabu Fighter Ameongea Kuhusu Nay Wa Mitego Na Mabaunsa

Mwarabu Fighter amempongeza Nay wa Mitego

Aliyewahi kuwa kuwa bodygard wa msanii DiamondPlatnumz, Mwarabu figheter amempongeza msanii wa muziki wa bongofleva Nay wa mitego baada kuongelea mabaunsa wanaowalinda wasanii wasiokuwa na vigezo vya kulindwa. Mwarabu fighter amesema kuwa kitendo cha mabaunsa kuwalinda watu wasiopaswa kulindwa ni kuivunjia heshima tasnia ya ulinzi.
Mwarabu amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha radio kiitwacho Mid Morning Fresh cha +255 Global Radio kinachorusha matangazo yake kutoka Sinza Mori Dar es salaam Tanzania.

 

Amesema kuwa anapongeza Nay wa mitego kutokana na kauli yake kwa mabaunsa wanaoishushia hadhi tasnia ya ubodyard.
Pia amesema kuwa ameamua kuanzisha kampuni ambayo inashughulika na masuala ya ulinzi ili kuweza kulinda vigezo vya kiusalama ili kuweza kuondokana na mabaunsa wasio na vigezo


Vilevile amekanusha taarifa zilizowahi kusambaa kuhusu kile kinachosemekana kujihisisha kimapenzi na mpenzi wa msanii wa muziki wa bongofleva Harmonize (Sara) kuwa haukuwa ukweli wowote ni uzushi tu wa watu.

 2,586 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey