Sambaza

Nicki Minaj Kuhusu Kolabo Na Adele

Nicki Minaj aliwahi kuwaambia mashabiki wake  kama kuna uwezekano akafanya kolabo na Adele, lakini inaonekana kama mastaa hao bado hawajawahi kukutana ili wafanye ngoma ya pamoja.

Kwenye moja ya interview aliyofanya wikiendi iliyopita, Nicki Minaj alisema ,“Yes and yes, yes and yes, wohoo!”, Lakini Adele alinifanya nijiapize kutomwambia mtu kama nimefanya naye kazi”

Jibu hilo la Nicki Minaj lilipata mapokeo makubwa ya mashabiki na kuzua mjadala ambapo baadae iligundulika Nicki Minaj alikuwa anafanya utani na kauli hiyo haikuwa na ukweli ndani yake.

“Omg. Nilidhani kila mtu anaweza kuona wazi kuwa nilikuwa mchekeshaji. S – t!, Sasa lazima niende studio ya Adele na kuiba faili kadhaa. Nani yuko Uingereza? Nimepata kazi kwa ajili yake. “aliandika Nick Minaj kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya mjadala huo kuwa mkubwa.

Uvumi huu wa Nicki Minaj kufanya kolabo na Adele unaweza usiwe kweli na wakati huo ukawa ni wa kweli kwani wanamuziki hawa kila mmoja ni shabbiki wa mwenzake na kupitia Instastory, Nicki Minaj amekuwa akionekana kusikiliza nyimbo za Adele
Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey