Kolabo Ya Vanessa Mdee Na Rayvanny Ilisubiriwa Kwa Hamu, Bado Ni Wimbo Unaosikilizwa Mara Nyingi
Oktoba 14 kwenye kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vanessa Mdee alitoa wimbo wake mpya ‘Bado’ aliomshirikisha Rayvanny wa WCB Wasafi.
Kwa mujibu wa BoomPlay, Bado ndio wimbo unaosikilizwa zaidi wiki hii kwenye chati ya nyimbo 100 zinazosikilizwa mara nyingi Tanzania, Tumeongea na Marketing Manager wa BoomPlay Faith Hillary aliyefafanua jinsi chati hiyo inavyofanya kazi na imekuwaje mpaka wimbo wa Vanessa Mdee umekuwa wa kwanza ndani ya siku mbili ikiwa kuna ngoma nyingine kali zilizokuwepo kabla yake. Faith amesema kigezo kinachotumika wimbo kuwa namba moja kwenye chati ya nyimbo 100 zinazosikilizwa wiki nzima, ni idadi ya wasikilizaji pamoja na engagement ikihusisha komenti na idadi ya downloads.
Faith amesema wimbo wa Vanessa Mdee na Rayvanny uliachiwa na BoomPlay peke yake ambapo mashabiki walikuwa na uwezo wa kuusikiliza bila kuudownload kitu kilichoufanya utimize vigezo vyote na kupata wasikilizaji wengi ndani ya muda mfupi.
“Tunaweza kuset kwenye system yetu kutokana na makubaliano na msanii mwenyewe mpaka atakapotaka kuiachia kwenye platforms nyingine kitu ambacho kimechangia wimbo huu kuwa engaged mara nyingi, so tulikubaliana hivyo na Vanessa mpaka leo ambapo imeachiwa rasmi “. alisema Faith Hillary
Kuhusu nyimbo zinazosikilizwa sana kwenye mtandao huo, Faith amesema wasikilizaji wengi wa BoomPlay wanapenda kusikiliza nyimbo za dini that’s why hadi leo wimbo wa Walter Chilambo ‘Only You’ upo nafasi za juu licha ya kuwa uliachiwa April 2018, hivyo haijalishi ni wimbo wa mwaka gani, wimbo unaweza kuwa na miaka mitatu lakini unasikilizwa na watu wengi ndio maana unaingia kwenye chati hiyo.
Kwa mujibu wa chati hiyo ambayo imekuwa updated Jumatano (Oktoba 16), Mimi Mars anasikilizwa kwenye nafasi ya pili akifuatiwa na Hello ambayo ni kolabo ya Ommy Dimpoz na Mwana F.A ,Kutokea nafasi ya kwanza wiki iliyopita, Yope Remix ya Inno’s B na Diamond Platnumz wiki hii imekaa kwenye nafasi ya nne, nafasi ya tano ni Kiza kinene ya Nandy na Sauti Sol ambayo inaikamilisha Top 5 ya nyimbo 100 zinazosikilizwa mara nyingi Tanzania.
Bado ni wimbo wa pili kutoka kwenye Expensive, EP ya Vanessa Mdee aliyoitangaza wakati anaachia hitsong yake ya mwaka huu ‘Moyo’. Kwenye intavyuu na +255 Global Radio, Vanessa Mdee alisema EP hiyo yote imefanywa production na S2kizzy ambaye alihusika kuisuka Moyo, Tuendelee kufurahia ‘BADO’ kabla Vanessa hajaidropisha EP yake yote ambayo inaonekana kucheleweshwa kama ilivyokuwa kwenye albamu yake ‘Money Mondays’ ambayo ilitoka miezi mingi baada ya kutangazwa ujio wake kisha ikavunja rekodi nyingi za muziki wa Afrika Mashariki..
Hii hapa ni Lyrics Video ya BADO Feat. Rayvanny
4,957 total views, 6 views today