Sambaza

Baada Ya Kuachana, Travis Scott Na Kylie Jenner Hawawezi Kukaa Mbali

Kufuatia ripoti za kutengana kwao mwezi uliopita, Travis Scott na Kylie Jenner wanaonekana kukosa uvumilivu kutokana na kinachoendelea.

Mashabiki wa Travis Scott wanadai kuwa Rappa huyo alitupia instastory iliyokuwa ikimuonyesha binti yake Stormi akicheza muziki huku pembeni ikisikika sauti ya mtu anayedhaniwa kuwa ni Kylie Jenner.

Mashabiki walikuwa surprised kusikia sauti ya Kylie ambaye hakuonekana kwenye video hiyo, kitu ambacho kilileta tafsri ya familia hiyo kutenga muda wa pamoja licha ya kuwepo taarifa kama hawapo kwenye mahusiano ya mapenzi tena.

Mara ya mwisho wawili hao kuonekana pamoja ilikuwa mwezi Agosti kwenye uzinduzi wa filamu ya Travis Scott inayoitwa ‘Look Mom I Can Fly’, Kuanzia hapo, mahusiano yao yalitajwa kupoa mpaka walipoamua kuchukua breki.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey