Elton John Asema Michael Jackson Mwishoni Alichanganyikiwa
Sir Elton John mwanamuziki nyota wa Uingereza amesema hayati bingwa wa muziki wa pop, Mmarekani Michael Jackson aliyamaliza maish akiwa amechanganyikiwa.
Akizungumzia kuhusu kitabu cha kumbukumbu za Michael kiitwacho ‘Me’, Elton (72) amesema “nilimfahamu Michael tangu akiwa na umri wa miaka 13 au 14… Alikuwa ni kijana mtanashati, lakini baadaye alianza kujitenga na dunia na ukweli kama alivyofanya mwanamuziki hayati Elvis Presey… Mungu anajua nini kilikuwa kichwani mwake kilichomfanya kuanza kutumia madawa ya kila aina na kupoteza kabisa taswira na haiba yake.”
Elton aliongeza: “Sisemi kwa utani… Alikuwa amechanganyikiwa kabisa.” Anaendelea kusimulia kwamba kuna siku Elton alimkaribisha nyumbani kwake, akaondoka kidogo na kumkuta anacheza na mtoto wa mlinzi wa nyumba yake.
“Alikuwa amechanganyikiwa, hakuweza kuishi na watu wazima,” anaongeza.
Michael Jackson alikufa ghafla kwa kuzidisha madawa ya kupunguza maumivu aliyopewa na daktari wake, Conrad Murray.