Sambaza

Kaka wa Nicki Minaj Hatiani kwa Kubaka Kibinti Miaka 11

KAKA wa rapa Nicki Minaj ametiwa hatiani kwa kubaka kibinti cha umri wa miaka 11 nyumbani kwake huko Long Island, Marekani. Jopo la wazee wa mahakama lilitoa hukumu jana dhidi ya Jelan Maraj (38) ambako atakabiliwa na kifungo cha maka 25.

Kisichana hicho ambacho sasa kina umri wa miaka 14 kilisema jamaa alikaibaka kila mara kwa miezi minane nyumbani kwake mwaka 2015 huko Baldwin.

Upande wa mashitaka umethibitisha madai hayo kupitia vinasaba, na kaka mdogo wa kibinti hicho alisema aliwahi kushuhudia shambulio moja kati ya matukio hayo ya ubakaji. Wanasheria wa Maraj wamesema madai hayo yamepikwa ili kumfanya Nicki Minaj alipe dola milioni  25 (Sh. bil. 57.4). Maraj na dada yake hawajatoa ushahidi wowote.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey