Sambaza

Joh Makini Afunguka Kuachia Ngoma na Falz Kutoka Nigeria

Msanii mahiri wa muziki wa HIP HOP hapa nchini, John Simon maarufu kwa jina la Joh Makini, amesema hajaamua kuachia ngoma yake mpya na Msanii Folarin Falana ‘Falz’ kutoka Nigeria akieleza si lazima kufanya collabo na msanii wa nje ya nchi.

Akizungumza na +255 Global Radio kupitia Bongo 255, Makini amesema si lazima kuwashirikisha wasanii wa kimataifa sababu yeye mwenyewe ni wa kimataifa.

Makini amefunguka kwa kusema kuwa ili kuonekana msanii uko levo za kimataifa si lazima kufanya collabo na wasanii wa nje.

Mkongwe huyo katika tasinia ya HipHop amesema watu wengi wamejijengea ili uonekane kuwa ni kimataifa basi unapaswa kufanya kazi na msanii wa nje kitu ambacho si sahihi.

“Si lazima msanii wa Tanzania afanye collabo na msanii wa nje ndiyo uonekane kuwa ni wa kimataifa.
“Wengi wamejijengea kuwa ukifanya collabo na msanii wa nje ndiyo unaonekana wewe ni wa kimataifa.
“Tunaona wasanii wengi wa nje wanafanya nyimbo na wazawa wenzao kama Nigeria, hivyo kuhusu kutoa nyimbo na Falz naweza nisiitoe kabisa,” alisema Makini.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey