Nicki Minaj Afunga Ndoa na Kenneth Petty
RAPA nyota Mmarekani, Nicki Minaj (36), hivi sasa ni mke kamili wa rafiki yake wa siku nyingi, Kenneth Petty (41). Hii inafuatia ndoa ya siri waliyoifunga tarehe 20 mwezi huu (Oktoba).
Minaj alitangaza hayo baada ya kuweka video katika mtandao wa Instagram ikionyesha vikombe vikubwa na kofia, vya rangi nyeusi na nyeupe vilivyoandikwa “Mr. and Mrs.” (Bwana na Bibi) na “Bride” and “Groom” (Bibi na Bwana Harusi).
Toa Maoni Yako Hapa