Sambaza

Vanessa ndani ya penzi zito na Mnaigeria

 Rotimi

MWANAMUZIKI staa wa Nigeria, Rotimi, hivi sasa yuko chanda na kidole na kimwana wa Tanzania, mwimbaji na mtunzi,  Vanessa Mdee, anayejulikana pia kama Vee Money.   Mrembo huyo wa haja pia ni mwanaharakati na nyota wa televisheni akiwahi pia kuwa mmoja wa majaji wa  mpambano wa kutafuta vipaji Afrika Mashariki ujulikanao kama  “East Africa’s Got Talent.”

Wawili hao hivi sasa wanakula bata huko Miami, Marekani.

Katika kuthibitisha ukaribu wao, wame-post katika mtandao wa Instagram video ikiwaonyesha walipokuwa katika bwawa moja.

Yote kwa yote, lazima kuna kitu kati ya nyota hao.  Kilichobaki ni kusubiri, kitaeleweka!

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey