CARDI B AJIUNGA NA FILAMU YA ‘FAST & FURIOUS 9’
RAPA Mmarekani, Cardi B kajiunga na mchakato wa muvi ya Fast & Furious 9 ambayo inategemewa kutinga katika majumba mbalimbali ya sinema mwaka kesho.
Nyota wa muvi hiyo, Vin Diesel, alimfichua memba mpya katika muvi hiyo kwa kum-posti katika mtandao wa Instagram siku ya mwisho ambapo ‘shooting’ ya mkanda huo ilikuwa ikifanyika nchini Uingereza.
“Leo inatimia siku ya 86 katika kuitayarisha Fast 9. Najua nimechoka, hata hivyo tulitoa kila juhudi kufanikisha muvi hii,” alisema Diesel.
Hapo ndipo Cardi, aliyekuwa amevaa vesti nyeusi na glovu nyeusi alipoungana naye akisema: “Nimechoka, lakini siwezi kusubiri zaidi. Nina uhakika hapa itatoka kazi nzuri zaidi.”
Cardi amewahi kushiriki katika muvi iliyochezwa na nyota Jennifer Lopez, Constance Wu, na Keke Palmer iitwayo Hustlers ambayo iliingiza mkwanja mkubwa.