Sambaza

Mwigizaji Lupita Nyong’o: Sina nia ya kuingia katika siasa

MSHINDI wa tuzo ya filamu ya Oscar, mwigizaji  Lupita Nyong’o, amesema hana nia ya kufuata nyayo za kisiasa za baba yake, Gavana wa Kisumu,  Anyang’ Nyong’o.

Akizungumza na jarida la Vanity Fair la London, Uingereza, alisema pamoja na kuzaliwa katika familia ya kisiasa na kwamba “baba alikuwa anapigania kile alichokiamini”, alisisitiza kwamba mwanasiasa mmoja katika familia moja anatosha.

Lakini alisema pia kwamba: “Nafikiri hilo lilinijaza hisia za kutambua kwamba kuna mambo kadhaa duniani ambayo yanabidi yabadilishwe…dunia ambayo tunataka kuwa sehemu yake.”

Hata hivyo, Lupita anasema anaweza kucheza nafasi za kisiasa katika filamu hii ni pamoja na anapokumbushia alivyocheza katika filamu ya Black Panther iliyoingiza mkwanja wa Dola bilioni 1.347, na kuwa ya mafanikio makubwa duniani.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey