Ngoma Mpya ya Selena ni Dongo kwa Bieber? – Video
Mwanadada Selena Gomez ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Supr Star wa Pop nchini Marekani, Justine Bieber, ameachia video ya ngoma yake inayoitwa “Lose you to love me” na kusababisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii.
Kama inavyotegemewa kutoka kwa mashabiki katika mitandao ya kijamii, kipindi Selena Gomez anaachia kibao chake kipya usiku wa Jumanne, walikuwa wakitafuta kujua ukweli kuhusu kibao hiko.
Inaonesha inamuhusu Justin Bieber, walisikika. Kibao hiko kinahusu mahusiano mabaya ambapo kinanatafsiri Selena ameyaepuka, ameyapitia na kuwa imara Zaidi.
Toa Maoni Yako Hapa