Sambaza

Rihanna, Drake Mhhh! Ammwagia Mapochopocho

Mshindi wa tuzo za Grammy, Drake ameibua gumzo mitandaoni wakati wa hafla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa juzi Jumatatu, Oktoba 22, 2019 usiku baada ya kukutana na rafiki yake ambaye pia ni rapa maarufu duniani, Rihanna.

Drake ambaye hit-maker wa nyimbo “Hotline Bling” na wanakikundi wa Lebo yake ya OVO alitinga katika klabu ya usiku ya Poppy ambapo pia alikuwepo Rihanna akila bata.

Rihanna alikuwa na kampani ya marafiki wake wa kike wawili huku wakiongozwa na walinzi, walielekea kwenye meza alikokaa Drake.

Rihanna na Drake waliongea, wakatabasamu na wakacheka kwa muda lakini mazungumzo yao yalibaki kuwa ni siri yao. Baada ya tukio hilo la muda mfupi, Rihanna na marafiki zake walisepa maeneo hayo.

 

Mmoja wa marafiki wa walioambatana na Rinahha aitwaye Lyrica Anderson aliposti picha kwenye Instagram Story yake na kumsifia rihanna alivyokuwa akicheza na drake. Lyrica anasema ulikuwa usiku mzuri kwa Rihanna na marafiki zake kwani walipewa zawadi za kutosha alizokuja nazo Drake. “When Drake brings McDonald’s to the club,” aliandika Lyrica.

 

Tangu mwaka 2016, Drake na Rihanna wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye mahusinao ya kimapenzi lakini wao hawajawahi kuthibitisha tetesi hizo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey