Selena Gomez akanusha wimbo wake kumlenga Bieber, mkewe Hailey
MWIMBAJI Selena Gomez amekanusha kwamba hajatunga wimbo uliomlenga mshikaji wake wa zamani, Justin Bieber ili kumuudhi mkewe, Hailey.
Wimbo huo wa ‘Lose You To Love Me’ umemfanya Hailey, kutupia ujumbe kwenye mtandao wa Instagram kuhusu ’tishio la kuua’, jambo ambalo limepindishwa baadaye kwamba ujumbe huo haukumlenga Gomez.
Hata hivyo, Gomez amesema alikuwa amenuia kuandika wimbo huo kwa hisia ambazo hazikutia maanani mtengano wake na mshikaji huyo wa zamani.
Toa Maoni Yako Hapa