Sambaza

Kanye Aianika ‘Jesus is King’

Kanye West ameianika orodha ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake inayosubiliwa kwa hamu, ’Jesus is King’ ambapo inaonesha orodha ya nyimbo tofauti na aliyoitoa mke wake Kim Kardashian mnamo mwezi wa nane.

Ingawa  bado hajaweka wazi kuhusu tarehe rasmi ambayo ataachia albamu hiyo, Kanye amewahakikishia kila mmoja kuwa albamu hiyo ataiachia soon.

Orodha hiyo imepungua wimbo mmoja kulingana na orodha ya awali aliyoitoa Kim huku kukiwa na mabadiliko katika majina ya nyimbo, ingawa majina manne ya nyimbo zilizopo kwenye orodha ya Kim yamebaki katika orodha ya Kanye.

Baadhi ya nyimbo zenye majina mapya ni ‘Follow  God,’ ‘On God,’ ’Everything We Need,’ ‘Use The Gospel,’ and ‘Jesus is Lord.’

Kanye aliahidi albamu yake mpya itahusisha zaidi masuala ya kidini, kama inavyojionesha ‘Jesus is King pamoja na mistari liyomo katika hizo nyimbo na kuokolewa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey