Sambaza

Mama Kanumba: Seth Sasa ni Mlemavu, Nisaidieni – Video

HIVI karibuni kumekuwepo na taarifa za ugonjwa wa mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aitwaye Seth Bosco, ambaye mpaka sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela.

‘Sina uwezo wa kumbeba na tayari Seth amekuwa mlemavu, yaani ameamka mzima aliniaga anakwenda kanisani nikamjibu sawa. Akiwa kanisani akainama kufunga kamba ya viatu, wakati ameinama akaskia kama shoti ya umeme mgongoni. Alivyorudi aliniambia alijisikia vibaya kanisani, nikamwambia achukue panado anywe. Jumatatu alikuwa hawezi tena wa kubebwa iliniumiza sana.

 

“Akasema mama spati choo, mama mkojo hautoki, mama miguu imekufa ganzi, tukampeleka Hospitali ya Palestina wakampima wakasema hatumuwezi nenda Muhimbili, tulipompeleka kule akamlaza Mwaisela akapimwa kwenye MRI na kusema ana uvimbe kwenye uti wa mgongo na kumuhamishia MOI. Walimfanyia operesheni na kutoa uvimbe huo lakini hali yake bado.

 

 

‘’Johari hili suala alilibeba aliwatangazia wasanii wengine na bili ya Mwaisela alilipia yeye Johari,’’ amesema Mama Kanumba.

 

Global TV Online imefika nyumbani kwa Mama Kanumba ambaye ndiye anayemlea Seth, na amesimulia hali yake ambayo ilianza ghafla tu akiwa anatoka kanisani.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey