Sambaza

Mama Kanumba: Watanzania Msaidieni Mwanangu Seth Bosco Anaumwa Amepooza – Video

Mama Kanumba, Flora Mtegoa.

Mama Kanumba, Flora Mtegoa, leo Ijumaa, Oktoba 25, 2019 amefika katika kipindi cha Front Page cha +255 Global Radio na kutoa pongezi kwa Kampuni ya Global Publishers, kupitia vyombo vyake vya habari vya Global TV Online na Global Radio ambapo watangazaji wake walifunga safari hadi nyumbani kwa mama Kanumba baada ya kupata taarifa za kuuguliwa na mwanae, Seth Bosco ambaye ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba.

 

Baada ya watangazaji wa kipindi hicho kufika nyumbani kwake, Mama Kanumba, aliezea hali halisi ya ugonjwa unaomsumbua Seth ambapo Watanzania walisikia kilio cha Mama Kanumba na kuanza kumsaidia.

Mama Mzazi  wa Steven Kanumba akiwa na watangazaji wa kipindi cha Front Page cha +255 Global Radio mapema leo alipokuja kutoa shukrani zake kwa uongozi mzima wa Global Publishers kutokana na kutoa habari  ya kuuguliwa na mtoto wake ambaye pia ni  mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco aliyepooza.

Ametoa pongezi kwa msanii mkongwe wa maigizo nchini Tanzania, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye alipopokea taarifa za ugonjwa wa Seth Bosco alimwambia Mama Kanumba kuwa peke yake hawezi, ndipo akaamua kuwashirikisha wasanii wenzake, Steve Nyerere, Ray Kigosi, Irene Uwoya na Irene Paul ambao walichukua hatua ya kulipia matibabu ya mwanae kwa awamu ya kwanza.

 

Mama Kanumba amewaomba Watanzania kumsaidia mwanae huyo matibabu pamoja na kiti cha magurudumu (Wheel Chair) kwa kuwa kwa sasa hawezi kutembea.

Kwa wanaoweza kumchangia wanaweza kutumia namba hii 0717 34 52 31 kuwasiliana na Mama Kanumba.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey