Sambaza

Irene Uwoya Amefunga Ndoa? Picha ‘zaiteka’ Insta – Video

Mitandao ya kijamii hususan Instagram leo imetapakaa picha za Staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya, zikionyesha akiwa amefunga ndoa na mwanaume ambaye hajafamika jina lake. Mastaa mbalimbali wameposti picha zake hizo wakimpongeza.

Walichokisema baadhi ya mastaa kupitia kwenye akaunti zao za Instagram:-

”I am Shocked!!!!!!!!!! @ireneuwoya8 please tell me is this Real!!!?? ?…….,” aliandika Mtangazaji Zamaradi Mketema.

“SIJAALIKWA NA KADI SIJAPEWA….(naelewa kiutu uzima) lakini @ireneuwoya8 I wish you nothing but the best mama, KAPANGA MUNGU, SIJASHUHUDIA LAKINI PICHA NAIONA SASA MIMI NANI KUPINGA??@loydemich najua I have a friend alienyuka designers only and hata kama sikupewa kadi but nimewakilishwa, BADO TU NATAKA KUJUA LEO NI AFTERPARTY YA NDOA? NI KURINGISHIWA CHETI?AU HIYO SUTI NA SURA? AU NI DINNER AU NI NINI???? KUKOMA LEO TUTAKOMAAAAAAAAA??26.10 I SAVED THE DATE?,” aliandika muigizaji Irene Paul.

Mdogo wangu Irene basi tusamehe sisi maana ndoa tatu mi dada akoo hata moja haya hongera tena @ireneuwoya8 #mambonimengimudamchache,” aliandika muigizaji Blandina Chagula ‘Johari’.

“Unajua we ni pacha wangu lakini kuna v2 Tumepishana kwenye kuuguza watu miyoyooo ?Naogoooopaaaa @ireneuwoya8,” alichangia muigizaji Jacqueline Wolper.

“@zamaradimketema Umemwaga Ugali wacha mimi nimwage mboga Amna namna, Haya family @efmtanzania Inakupongeza sana @ireneuwoya8 Tukutane Jioni Basi,” alichangia muigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Kabla ya tukio hilo lililofanyika leo na kutikisa mitandao ya kijamii, Uwoya alikuwa akiinadi siku ya Oktoba 26 kuwa itakuwa na sapraizi kwake kwa kuandika maneno ‘save date’.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey