Sambaza

Jux Kudropisha Albamu Yake ‘The Love’ Ijumaa Hii

After a very long wait na delay za kutosha, hatimaye Kanye West ameiachia Jesus Is king ambayo ni albamu yake ya tisa. Albamu hiyo yenye ngoma 11 za Gospo, iliachiwa usiku wa Ijumaa (Oktoba 25) na mpaka sasa nyimbo zake zinasikilizwa kwenye Top 10 ya mtandao wa Spotify.

Albamu hii imekuja sambamba na ujio wa filamu ya maisha halisi ya Kanye katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, filamu hiyo ambayo pia inaitwa Jesus Is King, ni moja ya vitu vinavyothibitisha kuokoka kwa Rappa huyo ambaye kipindi cha nyuma amekuwa akifanya mambo mengi kinyume na MUNGU.
Wakati dunia ikitia shaka juu ya wokovu wa Ye na trend ya Jesus Is King, Mashabiki wa muziki wa Bongofleva wanasubiri kwa hamu albamu ya African Boy JUX ambaye Jumapili (Otoba 27) alitumia instagram kuonyesha kava ya albamu yake yenye tracklist ya ngoma 18.

The  Love ni albamu ya kwanza ya JUX yenye kolabo na supastaaz kama Diamond Platnumz ambaye aliwahi kupost kipande cha video kikiwaonyesha wawili hao kwenye utengenezaji wa video. Diamond ameungana na Jux kwenye track #13 (Sugua) ambayo ni production ya Zombie S2Kizzy aliyehusika kwenye utengenezaji wa Sumaku na Vanessa Mdee, ngoma ambayo imepata nafasi ya kuwepo kwenye albamu ya JUX kwenye track #9.

Kwenye kolabo nyingine JUX amewakutanisha Gnako na Tommy Flavour kwenye mkwaju mwingine ulionyongwa na S2Kizzy, ngoma inaitwa Sugarcane ambayo sio mara ya kwanza kuwakutanisha Gnako na JUX lakini inakuwa mara ya kwanza kwa Tommy Flavour kufanya kazi na wote wawili kwenye ngoma hiyo ambayo imepewa track #7.
Ukiacha Sugua, Sumaku na Sugarcane, S2kizzy ametengeneza mikwaju mitano na ndiye prodyuza aliyefanya ngoma nyingi kwenye albamu hiyo zikiwemo Kibindoni, na Tell Me aliyoshirikishwa mwamba Joh Makini ambayo ni track #17.

During Tigo Fiesta Arusha, Ruby aliungana na JUX kuperfom ‘Juu’, ngoma ambayo JUX aliimba na Ex-Girlfriend wake Vee Money.. Kabla ya kuachia kava ya albamu hiyo jana, JUX alikuwa ameshathibitisha ujio wa kolabo yake na Ruby na tayari tumepata majibu kuwa ngoma hii ni track #4 itakwenda kwa jina la Wambera, Bob Manecky ambaye ni prodyuza wa muda mrefu wa JUX amehusika kuitengeneza kolabo hiyo, nyimbo nyingine alizotengeneza Bob Manecky kwenye albamu hiyo ni Zaidi, Incase You Don’t know, na Now You Know, track #16 ambayo ni kolabo ya JUX na legendari Q-Chief (Chillah) ambaye bila shaka anataka kuthibitisha kuna mengi baada ya The Return Of Q-Chillah, EP ambayo imempa platform ya kusikilizwa upya kupitia kolabo zake tatu na Harmonize Including My Boo Remix ambayo orijino yake ilibamba katikati ya miaka ya 2000 wakati ambao ulimwengu wa muziki haukutegemea kuwasikia Harmonize wala JUX ambao now wanatoa heshima kwa kuunganisha mchango wa mkongwe huyo kwenye kazi zao.

According to tracklist ya #TheLoveAlbum, kuna intro inayofuatiwa na ngoma 17, ngoma 11 kati ya zote hazijawahi kusikika, kuna ngoma tano ambazo tumewahi kuzisikia pamoja  na bonus track moja, ‘Umenibamba’ iliyotengenezwa na Luffa na ndiyo inayofunga tracklist hiyo.
Wapenzi wa gitaa na saxophone mjiandae kufurahia muziki mzuri kwani albamu hii ina ngoma nne kwa ajili yenu.
#TheLoveAlbum itaanza kupatikana Novemba 1,2019. Kwa wakati huu, mashabiki wa JUX na Bongofleva wanaweza kuweka order  na kuipata kwa wakati Albamu hiyo itakapoachiwa…PRE-ORDER|The Love Album By JUX.

 2,892 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey