Sambaza

Mzimu wa majina wamwandama P. Diddy, Atua mahakamani kubadilisha jina

 

Kwa mara nyingine tena, Rapper Sean John Combs almaarufu kwa jina la P. Diddy, ametangaza kubadilisha jina lake la kati ‘John’ na kuitwa LOVE kutokana na kubadilisha mfumo wa maisha yake. P. Diddy ameamua kutoa jina la ‘John’ na kutumia Love, Kwa madai kuwa kwa sasa hayupo tayari kutumia majina aliyokuwa anayatumia kama vile P.Diddy, Puffy, Diddy na Puff Daddy.

Kwa mujibu wa mtandao wa ET, P. Diddy tayari ameshawasilisha ombi lake la kubadilisha jina hilo katika Mahakama Mjini Los Angeles, Marekani. Rapper huyo mwenye miaka 49, Mwaka 2017 alitangaza kubadilisha jina lakini baadae akabadili mtazamo wake kutokana na sababu za kibiashara.

Nilikuwa  nimeamua kubadilisha jina langu kwa mara nyingine, hii ni kwa sababu maisha yangu kwa ujumla yamebadilika, Na ningependa kutumia jina la Love a.k.a Brother Love, Na sio majina mengine,” Alisema P. Diddy mwaka 2017 kabla ya baadae kuja kutangaza kuwa ameahirisha kubadilisha jina. Vyombo vingi vya habari nchini Marekani, Vimeripoti kuwa P. Diddy huenda akaanza kutumia jina hilo rasmi kwenye Birthday yake mwezi ujao Novemba 4, 2019.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey