Sambaza

Kigwangalla amkingia kifua Idris Sultan, sakata la JPM

Waziri wa Maliasili na Utalii; Dr. Hamisi Kigwangala, ameingilia kati sakata la mchekeshaji maarufu Idris Sultan anayetakiwa  kujisalimisha polisi baada ya kuhariri picha ya Rais Magufuli.  Agizo hilo la kujisalimisha polisi lilitolewa mapema leo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Waziri Kigwangala alitweet na kusema ” Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo.’

Hata hivyo mpaka sasa haijafahamika ni kituo gani mchekeshaji huyo ameenda kujisalimisha kufuatia kauli hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey