Sambaza

Mrembo wa Mombasa Afukuzia Penzi la Mbosso Dar

Msanii kutoka Label ya muziki WCB Mbosso Khan ameelezea namna ambayo aliweza kukwepa mshale wa mapenzi uliorushwa na mrembo mmoja aliyesafiri kutokea Mombasa Kenya hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuonyesha hisia zake za mapenzi kwa msanii huyo wa kiwanda cha muziki Bongo Flva.

 

Akizungumza katika Interview na Wasafi Media, Mbosso alielezea jinsi ambayo mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Munira, alivyorukia mbele ya gari lake nakudai kuwa anampenda na anahitaji kuwa naye kimahusiano.

 

Kulingana na tukio hilo Mbosso alituma moja ya wasaidizi wake kwenda kuchukua namba ya simu ya mrembo huyo na kumpa ahadi kuwa atawasiliana naye baadae. Hata hivyo hakuweza kumtafuta mrembo huyo akidhani ya kwamba amemuweza.

Kazi ya moyo sio tu kusukuma damu, kazi ya moyo pia ni kupenda. Unaambiwa mrembo huyo alizidi kumpenda Mbosso na kumfatilia kila kona anayokwenda. Ikijumuisha hadi katika nyumba ya Boss wa WCB, Diamond Platnumz; kumuulizia Mbosso mara kadha wa kadha.

 

Amekuwa msumbufu, ananipigia simu mara kwa mara na kwa namba tofauti tofauti. Nimewaambia watu wangu wablock namba zake zote. Mara ya mwisho kumuona ilikuwa katika geti la nyumba ya Diamond; nilikasirika kumuona pale nikamwambia aende nyumbani kwao. Alisema Mbosso.

 

Siwezi kuwa nae kimapenzi au kumsaidia kwa namna yoyote ile, kwasababu yeye ni mwanamke mgeni kwangu simfahamu na sitaki kukaribisha matatizo kwenye maisha yangu. Aliongeza Mbosso.

Anasema ananipenda, nisawa, lakini mambo huwa hayaendi hivyo. Unajua nina familia, nina mtoto, Itakuwa jambo la ajabu kwangu kurukia nakuingia kwenye mahusiano na mwanamke ambaye hata simfahamu. Aliongeza.

Mbosso alimaliza kwa kumshauri mrembo huyo arudi nyumbani kwao Mombasa, Kenya. Na labda anaweza kuja kumuoa hapo baadae baada ya kufuata taratibu sahihi.

 

“Ningependa kumshauri arudi kwao, akae na wazazi wake, huenda nitamuoa hapo baadae. Anajua wazi kuwa naweza kuoa wake hadi wanne.” Alisema Mbosso.

Alisema hayo baada ya Munira kuja kwenye hadhira na kutishia kuwa atasitisha maisha yake (kujiua) kama Mbosso atalitupilia mbali ombi lake la kumuoa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey