Sambaza

Wasafi Festival kutikisa Dar, Diamond amualika Harmonize na Alikiba ‘Show itaanza saa 1;00 asubuhi

Akianza na ratiba, Diamond amesema tamasha hilo litaanza saa 1:00 asubuhi siku ya Jumamosi Novemba 9, 2019 na litamalizika saa 6:00 usiku.

Kuhusu wasanii, Diamond amesema kutakuwa na aina zote za muziki, Watakuwepo wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wapya na wa zamani, Muziki wa Dansi, Singeli na taarabu.

Tamasha hilo ambalo litafanyika katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam, Huenda likahamishwa na kufanyika katika uwanja wa Taifa-Temeke endapo ombi la Diamond kwa Waziri Mwakyembe la kutumia uwanja huo litakubaliwa.

Diamond akiongea kwenye mkutano huo na Waandishi wa habari leo Oktoba 19, 2019, Aliuzwa pia kama msanii mwenzie Harmonize atapewa nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Kama unavyojua kila mtu anakuwa na ratiba tofauti tofauti, Lakini kama ratiba ikikaa sawa tunataka na yeye awepo. Tunataka wasanii tofauti tofauti wawepo, Boss Tale yupo Marekani lakini kabla ya kuondoka alimpigia simu Alikiba naye awepo,” amesema Diamond.

Tamasha la Wasafi Festival 2019, tayari limeshafanyika takribani mikoa 7 Tanzania bara ikiwemo Iringa, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga na Dodoma.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey