Nandy Awasili na Tuzo Yake Kutoka Marekani
STAA wa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania House of Talent (THT) The One and Only African Princess Fausta Charles Mfinaga, Nandy amerejea nchini akiwa na Tuzo yake ya AEAUSA aliyoibuka mshindi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nandy amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere, jijini Dar es Salaam akitokea New Jersey nchini Marekani ambako tuzo hizo zilifanyika usiku wa Oktoba 19, 2019 na kuibuka mshindi katika Kipengele cha Best Female Artist East/South/North Africa.
Msanii huyo ambaye ni Hitmaker wa Ngoma kama Ninogeshe, One Day, Nikumbushe, Hazipo, na nyingine kibao amepokelewa na nyomi la mashabiki waliofika uwanjani hapo kumlaki na kumpa pongezi kwa kuibuka mshindi wa tuzo hizo kubwa duniani.
Toa Maoni Yako Hapa