Sambaza

Dullvani, aomba kufundishwa mipaka ya sanaa

Comedian machahari hapa Tanzania anayefahamika kwa jina la Dullvani ameomba mamlaka husika zinazosimamia masuala ya maadili kwa wasanii kutoa elimu zaidi kuhusu kazi zao za mitandaoni.

“Wazidi kutupa elimu ili tujue mipaka yetu ni ipi, Hata kama ipo wajaribu kutufahamisha na kutuelimisha.” Alisema Dullvani


Dullvani amesema hayo leo alipokuwa akipiga story kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh cha +255 Global Radio.

Hii inafuatia baada ya hivi karibuni Mchekeshaji nguli na pia mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014 Idris Sultan kufanya utani kwa kuhariri picha Rais, tukio hilo likamueka matatani na kutakiwa kuripoti kituo cha polisi, kutokana na kitendo chake cha kuhariri picha ya Rais; Order hiyo ilitolewa  na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (Paul Makonda) kwa kudai kuwa msanii huyo wa vichekesho (Idris Sultan) hajui mipaka  ya kazi yake.

:
24/7#Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani
:
Usisahau pia kupakua app ya Global Radio usikilize radio na upate habari,matukio na burudani 24/7 kupitia simu yako ya mkononi. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.globalradio.app

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey