Sambaza

Idris Sultan aripoti tena polisi, haya ndio makosa yake

Mchekeshaji  Idris Sultan ameripoti kituo cha polisi kati leo Ijumaa Novemba Mosi, 2019 na kuhojiwa kwa dakika 30 na kutakiwa kuripoti tena Jumatano Novemba 6, 2019.

Jana asubuhi, Idris aliripoti kituoni hapo na kuhojiwa kwa saa tano na kupekuliwa nyumbani kwake,  usiku aliachiwa kwa dhamana akitakiwa kuripoti tena  leo saa 2 asubuhi, jambo ambalo amelitekeleza.

“Idris ameripoti kituoni saa 2:00 asubuhi na kuhojiwa kwa dakika 30. Wamechukua simu zake kwa uchunguzi na kutakiwa kuripoti tena Jumatano ijayo (Novemba 6, 2019).”

“Wamemueleza kuwa kosa lake ni kusambaza habari za uongo chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao. Kosa la pili ni kujifanya Rais chini ya kifungu cha 15 cha makosa ya mtandao,” amesema, Benedict Ishabakaki ambaye ni mwanasheria wa mchekeshaji huyo.

Jana alipopekuliwa nyumbani kwake polisi walichukua kompyuta mpakato kwa ajili ya uchunguzi, aliporudishwa kituoni kabla ya kupewa dhamana alipelekwa kitengo cha makosa ya mtandaoni

Juzi mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimtaka Idris kuripoti polisi  baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa.

Pia, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani.

Hata hivyo, dakika chache baada ya Makonda kumtaka msanii huyo kuripoti polisi, waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliahidi kumuwekea dhamana iwapo angekamatwa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey