JULIUS MTATIRO; Kabla sijafa natamani kuona kolabo ya Alikiba na Diamond
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amesema kabla hajafa angependa kuona wimbo wa pamoja/kolabo kati ya Diamond na Alikiba
Alisema; Hawa rafiki zangu Alikiba na Naseeb, kwanza ni vijana ambao kwenye eneo la mafanikio ni Role Models kwa vijana wa kitanzania, kuna mambo mengi ambayo wanaweza kuyafanya halafu yakawafanya wasiwe Role Models, kwasababu kuwa Role Model ni aspect (tukio) fulani wewe kama mwanadamu umeweza kufanikisha nini, kwahiyo mapungufu yako huwa hatuyabebi kama mifano mizuri ila tunaangalia yale mambo chanya na hayo ndio hua tunayabeba.
“Diamond amefanikiwa kimuziki na pia anaonekana kufanikiwa kiuchumi vivyo hivyo pamoja na mwenzake Alikiba. Nadhani mimi ni kati ya viongozi wanaopenda kusikia kolabo kati ya Diamond na Alikiba, na ninataka ujumbe huu uwafikie. Nimeshamwambia Naseeb, sijapata nafasi ya kukutana na Alikiba ila siku nikipata nitamwambia ; kuna mambo wala hayatusaidii haya mabifu, sisi tuna watazama kama wanamuziki wazuri, wana vipaji, wana nguvu , wana uwezo wa kufanya mambo makubwa.” Aliongeza.
Moja kati ya ndoto yangu kabla sijafa ningependa kuona wimbo wa pamoja kati ya Alikiba na Diamond, Sioni kama hii mipasho yao inawasaidia , badala yake wange concentrate kwenye kazi zao zaidi.
Mtatiro alizungumza hayo wakati alipokuwa akipiga story ndani ya kipindi cha Mwendo Kasi kutoka 255 Global Radio.