Sambaza

Aliyemtumia Meseji Marehemu Baba Yake, Ajibiwa Baada ya Miaka 4

Mrembo mwenye umri wa miaka 23, Chastity Patterson, aliachwa katika hali ya mshangao baada ya kupokea meseji kutoka kwenye simu (namba) ya marehemu baba yake baada ya kuwa anamtumia meseji kwa miaka minne mfululizo

Mara kadhaa Chastity alikuwa akituma ujumbe kwenda kwenye namba iliyokuwa ikitumiwa na marehemu baba yake, Jason Ligons’ kumjulisha maisha yake ya sasa kama namna ya kutunza kumbukumbu. Sasa basi Juma lililoisha, siku moja kabla ya kumbukumbu ya miaka minne toka kitokee kifo cha Baba yake; Chastity alituma ujumbe uliosomeka kama ‘Hey Dad, it’s ME. Tomorrow is going to be a tough day again!’ ( Baba, ni Mimi. Kesho inaenda kuwa siku ngumu tena!’)

Kwa Chastity ukaja mshangao baada ya mwanaume kwa jina la Brad kujibu ujumbe huo, akielezea namna ambayo alimpoteza Binti yake mwaka 2014. Na meseji zake zimekuwa zikimgusa sana.

Baada ya kupokea ujumbe toka katika simu ya Baba yake, Chastity alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. kuwa majibu yale yalionyesha dhahiri Baba yake yupo katika eneo la amani.

Ujumbe wa Brad ulikuwa kama hivi. ‘Habari mpenzi, Mimi sio Baba yako, ila nimekuwa nikipokea meseji zako kwa takribani miaka minne sasa. ‘Kawaida natazamia kupokea meseji zako kila asubuhi na kila usiku.’

‘Jina langu ni Brad na nilimpoteza Binti yangu kwenye ajali ya gari iliyotokea August 2014. Kila mara unapotuma meseji, najua ni meseji kutoka kwa Mungu. Nasikitika kuwa umempoteza mtu wa karibu sana kwako, Ila nimekuwa nikikusikiliza zaidi ya miaka kadhaa na nimekuona ukikua na ukiwa mtu wa tofauti kulinganisha na wengine.’

‘Nilitaka kujibu meseji zako miaka ya nyuma, ila sikutaka kukuvunja moyo.’

Akaongeza: ‘Wewe ni mwanamke wa kipekee na ninatamani binti yangu angekuwa kama ulivyo wewe, asante kwa meseji zako za kila siku, umenikumbusha kuwa kuna Mungu na haikuwa makosa kwa binti yangu kuondoka.’

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey