Sambaza

Idris amtoa chozi Lulu Diva!

SEXY lady wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ hivi karibuni alijikuta akidondosha chozi kufuatia msala alioupata mchekeshaji, Idris Sultan wa kuitwa polisi kutokana na ‘kuchezea’ picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ vibaya na Nembo ya Taifa.

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Lulu Diva alisema hakuna siku ambayo alilia kwa uchungu kama siku ambayo mchekeshaji huyo alipoingia mahabusu na kutoka kwa dhamana.

“Unajua kuna wakati ninafanya utani sana, lakini ukweli ni kwamba siku Idris alipoingia mahabusu niliumia sana kwa sababu ni ndugu yangu wa damu, lakini sikuwa na jinsi ya kufanya lolote,” alisema Lulu Diva.

Mwanadada huyo aliendelea kueleza kuwa, kikubwa kwa upande wake anamuombea kaka yake huyo amalize salama msala huo na anaamini ataumaliza vizuri.

Kinachotakiwa na ninachofanya kwa sasa ni kumuomba Mungu amvushe Idris salama kwenye hili, hivyo nina imani kwamba litapita tu kwa namna yoyote ile,” alisema Lulu Diva ambaye yeye na Idris ni ndugu.

Wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alimtaka Idris kuripoti kituo cha polisi baada ya kuweka picha ya Rais yenye sura yake huku akiwa ameketi kwenye kiti chenye Nembo ya Taifa.

Idris alitii agizo hilo na kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako alifanyiwa mahojiano na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Novemba 6, mwaka huu.

Cc: Ijumaa Wikienda

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey