Sambaza

T.I ampa somo Iggy Azalea

R APA Clifford Harris ‘T.I’ amempa somo staa wa kike kunako gemu la Hip Hop kutoka Marekani, Iggy Azalea kuwa anatakiwa kubadilika na siyo kuegemea kwa mashabiki Wazungu tu. T.I aliyasema hayo katika Kipindi cha The Breakfast Club kinachoruka kupitia TV ya Revolt kuwa, mwanzoni Iggy alijiona anapendwa sana na Wazungu akasahau kama kuna rangi nyeusi pia. “Alivyoona anapendwa na Wazungu hakutaka kabisa kuwajua watu weusi lakini kwa sasa amebadilika na kuwa penda wote. “Ninachotaka kumwambia, afanye vitu kwa tofauti asiegemee upande mmoja. Fanya kitu watu ndiyo wajivunie kuwa na wewe,” alisema T.I.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey