T-PESA, JERO TU UNAPATA DAKIKA, MESEJI, DATA ZA KUTOSHA – VIDEO
Je, umekuwa ukipata tabu kuhusu mawasiliano, SMS hazitoshi, Dakika hazitoshi na MB’s (bundles) hazitoshi? Unashindwa kuperusi… Basi hii ni taarifa njema kwako, kwani T-PESA imekuja na kampeni kubwa kuliko ambayo hutakiwi kupitwa wala kubaki nyuma.
Mchongo uko hivi, T-PESA sasa wanakuletea Bando Tam Tam la T-Pesa ambalo limekuja kuleta mapinduzi ya mawasiliano kwa gharama nafuu. Kwa bei chee kuanzia Shilingi 500 unapata Dakika, SMS pamoja MB’s za kutosha, haina haja tena kuazima azima simu kupiga, kutuma SMS na kuperuzi mtandaoni; kwa kupiga *150*71# unaweza kujiunga na kifurushi hicho kitamu kutoka TTCL
Akizungumza na kituo cha +255 Global Radio leo Jumanne, Novemba 5, 2019, Meneja Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mruta Hamis ameitambulisha rasmi Bando Tam Tam la T-Pesa kutoka TTCL ambayo imelenga kutatua changamoto za mawasiliano nchini na kuwapata wateja wake kitu cha tofauti huku wakifurahia mawasiliano ya kuongea, meseji na bando na vifurushi vya MBs kwa bei rahisi kuliko mtandao mwingine wowote nchini.
“Tanzania ni nchi yetu, TTCL ni shirika la umma, hivyo tunapenda kutambulisha na kuleta huduma mpya kutoka TTCL na huduma ni ‘Bando Tam Tam la T-PESA‘ ambalo limekuja kurahisha huduma za mawasilinao kwa watanzania wote na kwa gharama nafuu,” alisema Mruta.
“Ili kujiunga na huduma hiyo unapiga *150*71* unapata vifurushi vyote kuanzia vya siku, wiki mpaka mwezi kwa gharama ya kuanzia Tsh 500 hadi 5000, ambapo ndani yake utapata Dakika, SMS pamoja na Data ya kuperuzi mitandaoni. Watanzania turudi nyumbani, nyumbani kumenoga, Bando Tam Tam ni kwa ajili ya Watanzania,” alisema Msimamizi wa T-Pesa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ladislaus Komba.
Mbali na Mruta na Komba, wengine waliotembelea Ofisi za Global Group ni Ofisa Mahusiano TTCL Makao Makuu, Ester Venance Mbanguka na Ellyguard Katule na kujionea uendeshaji wa shughuli mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa vitengo mbalimbali ofisini hapo.