Drake kuja na kampuni hii ya kuuza Bangi
Kama wewe ni shabiki wa Drake basi basi fahamu kwamba Drake ameamua kuja na biashara hii mpya, kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Drake aliitambulisha kampuni yake mpya iitwayo “More Life Growth Company” lakini hakuanika wazi itakuwa inajihusha na nini.
Mtandao wa Hip Hop N More umebaini kwamba kampuni hiyo itajihusisha na kilimo pamoja na uuzaji wa zao la bangi. Kwenye maelezo yaliyoambatanishwa kwenye usajili wa kampuni hiyo yameweka wazi kuwa “More Life Growth Company” itahusika na Cannabis Products & herbs, medical herb extracts, herbal tea, Rolling papers, dried plants, Cigarette rolling Papers, Hookah tobacco, na mengine mengi. Swipe kushoto kusoma.
Drake anaungana na mastaa wengine kama Jay-Z, Wiz Khalifa na Post Malone ambao wanafanya biashara hiyo.