Sambaza

Miriam Odemba; Kuinua vipaji vipya vya Models

Miriam Odemba akizungumzia ‘Odemba Models Search’ ndani ya Studio za +255 Global Radio

MWANAMITINDO maarufu kutoka Tanzania Miriam Odemba amekuja na mpango wa kuinua na kuendeleza vipaji vya models wapya wa kitanzania, mpango huo unajulikana kama Odemba Models Search.

Akizungumza hayo jana 05 Nov 2019 kwenye kipindi cha Bongo 255 kutoka +255 Global Radio, Miriam alisema; “Nilikuwa nasumbuliwa sana na wasichana warembo ambao walitamani kuwa models ila wameshindwa kujiendeleza kuwa models  na wanataka kuwa kama mimi; Kwa kuwa mimi nina experience basi nikaamua kuja na hii Odemba Models Search ya kuweza kuwasaidia wasichana au ili vijana waweze kupata na kipato pia waweze kuwasaidia wazazi wao na zaidi waweze kujiendeleza wao zaidi na zaidi na Odemba ifike mbali.”

“Kama vile unaona kwa Diamond aliamua kuwa na Wasafi na inasaidia vijana waliopo pale; Nikasema why not!  hata mie Miriam Odemba I can, I can do that. Ndio sasa nimekuja na hii idea, i think ni idea nzuri sana na imepokelewa vizuri na wasichana na models, i think ninaweza kubadilisha maisha yao kama vile mimi nilivyoweza kubadilishwa maisha na Joseph Kusaga, Eric Shigongo pia marehemu Ruge na Amina Mungi.”  Aliongeza Miriam.

“Odemba Models Search imeanzisha rasmi mwaka huu na imedhamiria kuwainua na kuwaendeleza vijana wote wenye ndoto za kuwa models wakubwa.” Alimalizia Miriam.

Fahamu kwamba Miriam Odemba ni moja ya models kutoka Tanzania wanaofanya vizuri katika tasnia ya modeling kimataifa. Awali aliwahi kuwa Miss Temeke 1997,  Miss Tanzania 1998 (Top 10) , M-Net Face of Africa 1998 – (Top 5) ,  Elite Model Look Tanzania 1999 – (Top 17 at Elite Model Look 1999) , Miss Earth Tanzania 2008 , Miss Earth 2008 – (1st runner-up) Pia ameweza kushiriki majukwaa maarufu ya modeling Marekani na Ufaransa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey