Alikiba kuja na tamko rasmi
Kuelekea kwenye tamko rasmi kutoka kwa mfalme wa Bongo Flava Alikiba ameamua kuwaalika pia fans wake waweze kujumuika nae pindi atakapokua analifurumua hilo tamko, kupitia instagram page yake Alikiba ameandika hivi. . . “JE WEWE NI FAN NUMBER MOJA WA ALIKIBA?” Basi nina Kadi Mbili za mualiko kwa Fans wangu wawili katika #TamkoRasmi na #AfterParty – ili kuzipata niambie nina Miaka mingapi Katika Game ya Muziki, wimbo wangu wa kwanza ni upi nilio ingiza sauti na Kwanini unapenda Sana Muziki wangu . .
Je unafikiri Alikiba atakuja na tamko gani? Au amekubali Offer ya kufanya show ya Wasafi Festival? Mimi na wewe hatujui ila 255 Global Radio tuko hapa kukujuza kila kitachondelea kwenye tamko hilo.
Toa Maoni Yako Hapa