Sambaza

Producers wengi Bongo wanapenda rushwa ya ngono, Nini Tz afunguka

Nini Tz Msanii wa Bongo Fleva akizungumza jambo ndani ya studio za 255 Global Radio

Msanii wa Bongo Flava Nini Tz amefungaka na kuelezea changamoto alizowahi kukutana nazo toka ameingia rasmi katika muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)

Kupitia mahojiano aliyofanya na kituo cha Radio cha +255 Global Radio, Nini Alisema “Changamoto zipo hasa kwetu sisi watoto wa kike hasa pale unapotaka kwenda kurekodi wimbo wako studio, Rushwa ya ngono ipo na mimi ilishanikuta. Kuna wakati kama msanii unataka kwenda kurekodi na hali sio nzuri sasa producer anaingia na jambo hilo la kukutaka hasa wasanii wa kike ndio imekua tatizo.

Nini Tz Msanii wa Bongo Fleva akizungumza jambo ndani ya studio za 255 Global Radio

Alipoulizwa kuhusu mahusiano yake yeye  na Ney Wa Mitego, Alisema. Ney wa Mitego  ni boss wangu, mshikaji wangu, mtu ambaye hua na hang naye muda wote na pia  tunafanya kazi pamoja. Hivyo kwangu mimi sina haja ya kuficha mahusiano yangu watu walikuwa wanajua awali tulikuwa vipi.

Pia msanii huyo alipata nafasi ya kutambulisha wimbo ambao ameurudia kutoka kwa Msanii nguli Shaa

Nini Tz Msanii wa Bongo Fleva akiwa ndani ya studio za 255 Global Radio akitambulisha wimbo yake (Shoga Cover) ulio imbwa na Shaa.

“Shaa ni moja ya wasanii ambao nimekuwa nawasikiliza toka wakati nakua, Na ndio maana nikapenda kufanya cover kwenye wimbo wake wa Shoga, Nilikuwa tu studio nikasema nataka kufanya cover ya wimbo huo. Watu wangu wa karibu pia waliona ni nzuri na kubwa, unajua cover sio official song hii nimefanya kuonyesha uwezo mwingine  kwa kuanzia nataka kutoa hii ili watu waburudike nayo then baadae nitatoa kazi yangu mpya maana ni muda mrefu nimekaa bila kutoa kazi mpya.” Alisema Nini.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey