Sambaza

Kanye West awamaindi Forbes kwa kutomwita Bilionea

Kanye West kawaida amekuwa ni mtu ambaye yuko makini kuhusu utajiri wake, hasa lipofika suala la kuchapishwa kwa taarifa kuhusu ni kiasi gani cha pesa anaingiza kutoka kwenye biashara zake.

Katika maongezi yake kwenye Kongamano la Fast Company Innovation, Kanye West aliwamaindi Forbes kwa kutokumwita Bilionea licha kuwa aliwaonyesha Risiti ya Fedha yenye thamani ya dola milioni 890 (Trilioni 2 TZS) ambazo alizipata kama faida kupitia bidhaa yake ya Yeezy ila wakaamua kutokumpa heshima hiyo.

Kanye West hakuwa na raha juu ya jambo hilo kwani anafikiria ilikuwa ni kwa makusudi, Aliongeza kwa kusema “Martin Luther King hakuuwawa kwa sababu alikuwa na ndoto pekee, bali alikua na kitu kingine ambacho alikuwa akikisimamia ikiwa, uwezeshaji kwa watu weusi, uwezeshaji wa kiuchumi;  na hilo jambo watu hawapendi.”

“Wakati nafanya mazungumzo na Forbes niliwaonyesha risiti ya Dola milioni 890 na bado hawakusema mimi ni bilionea…hawataki kutuona tunaweza kununua ardhi, hawataki tuwe na umiliki 100%, na kwamba nina umiliki wa 100% wa Yeezy. Alisema Kanye West.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey