Young Killer & Young D vitani nani kuanza kutoa kazi mpya
Wasanii wa muziki wa HipHop ambao wanatajwa kuwa na tofauti Young Killer na Young Daresalama wamekutana studio kwa Mr T touchez na kuanza kubishana nani aanze kuachia kazi yake mpya
Kwa mujibu wa maelezo Young Daresalama anasikika akimwambia Young Killer amuache kwanza atangulie kuachia wimbo na kwa upande wa Young Killer anaonekana akisema hapana labda aanze yeye kuachia kazi
Wote hawa wana zaidi ya miezi minne toka waachie kazi zao rasmi ambapo Young Killer aliachia Chagamaa miezi minne iliyopita na Young D aliachia Gari Yangu Remix miezi mitano iliyopita
Toa Maoni Yako Hapa