Kevin Hart Awashukuru Mashabiki zake kwa mara ya kwanza toka apate ajali

Siku ya Jumapili (10 Novemba) mchekeshaji maarufu Duniani Kevin Hart alitokea kwa mara ya kwanza kwenye tukio la utoaji wa tuzo za People’s Choice, tangu alipolazwa hospitali baada ya kupata ajali mbaya ya gari miezi miwili iliyopita
Katika usiku huo wa tuzo, Kevin alitunukiwa tuzo ya Mchekeshaji bora wa mwaka “Comedy Act of2019”. Matandao wa USA TODAY umeripoti kuwa wakati Kevin alipokuwa akipanda jukwaani kupokea tuzo hiyo ukumbi mzima ulipatwa na msisimko kutokana na ujumbe alioutoa kugusa mioyo ya watu.
“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa sababu sina budi kuwa hapa,” Kuwa hivi nilivyo, inanifanya nithamini maisha zaidi, inanifanya nithamini vitu ambavyo ni vya muhimu. Nataka kumshukuru mke wangu na watoto wangu, Wamekuwa na mimi kweli kweli.” Alisema Kevin.
Mbali na kuishukuru familia yake na onyesho hilo la tuzo, pia alituma shukrani zake kwa mashabiki wake.
“Nawashukuru sana wote kwa kuwa pamoja nami katika wakati mgumu.” Aliongeza.
Msanii huyo alikuwa amekaa kimya kwa kitambo baada ya kupata majeraha makubwa kwenye mgongo wake baada ya gari yake aina ya Plymouth Barracuda kupata ajali mbaya na yeye akiwa ndani ya gari hiyo. Gari hiyo ilipoteza muelekeo na kupata ajali usiku wa manane mnamo Septemba 1