Kisa Ebitoke’ Mlela ayaoga mtandaoni
Muigizaji na mjasiriamali Esha Buheti, ameonekana kuchukizwa na kitendo alichokifanya Yusuph Mlela kwa kumsaliti Ebitoke na kumuonesha mpenzi wake mpya hadharani na kwenye mitandao ya kijamii.
Esha Buheti ameandika maneno makali kupitia mtandao wa Instagram, baada ya Ebitoke kugombana na mpenzi mpya wa Yusuph Mlela, katikati ya mkutano mbele ya waandishi wa habari uliofanyika siku ya leo Novemba 11.
Esha Buheti ameandika kuwa “Wanaume mpoje lakini, mbona kila siku kuumizana tu, wewe si ulimleta huyo ukaniambia ndiyo mwanamke wako, haya maisha ya ‘drama’ umeanza lini kwanza umri ushaenda tafuta mwanamke uoe kazi kuumiza watoto wa wenzio, nimeumia sana sio sawa kabisa upuuzi tu” ameandika Esha Buheti.
Aidha Buheti ameongeza kuwa, “Huna adabu kabla ya kumuumiza mtu jifikirie kwanza, nakuona mwenye akili kumbe mjinga na mwehu, mmezoea kutuumiza tunakaa kimya nimekuchukia Mlela mpaka natamani nikupike makange halafu mimi na Ebitoke tukule na ugali, hunibabaishi nje ndani mwanaume usio na nidhamu”.