“KONKO GANG MUSIC” Kuipeleka Hiphop na Bongo Fleva Inapostahili
KONKO GANG ni kampuni ya burudani inayomiliki kikundi Cha Muziki cha “KONKO GANG MUSIC” pamoja na kusimamia record Label ya muziki Mkoani Arusha ijulikanayo kama “IKO SAWA”.
KONKO GANG kama kampuni iko chini ya uongozi wa “Rick Lucas Thomas” a.k.a KONKO MASTER ambaye ameweza kua mstari wa mbele katika kukutanisha vijana wawili pamoja na yeye na kuunda kikundi Cha mziki wa kizazi kipya kijulikanacho kama “KONKO GANG MUSIC”.
Mpaka sasa ndani ya kikundi hicho kuna wasaniii watatu, ambao ni @dizafricana ama #Africana , @JustinCukaz ama #Cukaz pamoja na @rickthomasofficial ama #Konkomaster
Kundi Hili la mziki limeanzishwa mwaka 2019 na linapatikana jijini Arusha Ila bila mipaka linafanya kazi ndani na nje ya nchi.
Mpaka sasa kundi la “KONKO GANG MUSIC” limesharekodi nyimbo nyingi ndani ya studio za IKO SAWA na wengi waliobahatika kusikia nyimbo zao wanasema “ SASA HUU NDIO MUZIKI”.
Mpaka sasa kundi hili limetabiriwa kama kundi ambalo litaipeleka Muziki wa Tanzania katika atmosphere za kimataifa kutokana na utofauti wa kazi zao lakini pia ubunifu unaosikika ndani ya nyimbo zao.
KONKO GANG ina clothing line ijulikanayo kama KONKO Gang CL, Recording Studio, Management pamoja na haki Miliki ya nyimbo na bidhaa zao zote. Hili ni kundi la kwanza Tanzania kuweza kuweka rekodi ndani ya nchi ya kumilki kuanzia recording studio, video production, models pamoja na board of advisors ambaye mwenyekiti wake anajulikana kama “KING BERTO” ama Albert.
Kama kikundi Cha muziki KONKO Gang wamesha kamilisha Album Yao tayari na Muda si mrefu utapata nalala yako:
KONKO GANG ndio wasanii na kundi pekee walioaminiwa na kupewa nafasi ya kufanya matangazo ya TIGO FIESTA 2019.
Ombi Lao kwa Watanzania: MKAE TAYARI KWASABABU TUNAIPELEKA HIPHOP NA BONGO FLEVA INAPOSTAHILI.