Burna Boy kutoa mapato ya show kwa wahanga wa mashambulizi ya Xenophobia
Mwimbaji Burna Boy wa Nigeria ameripotiwa kwamba atatoa sehemu ya malipo yake ya tamasha la Africa Unite kwa waathirika wa mauaji ya wageni (Xenophobia) ambayo yalitokea miezi kadhaa nyuma.
Burna Boy alitangaza kurejea nchini Afrika Kusini na kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo litafanyika nchini Afrika Kusini mwezi huu. Awali aliapa kutokanyaga kabisa katika ardhi hiyo.
Toa Maoni Yako Hapa