Cissy Nansera’ Yoga imeokoa maisha yangu, nilikata tamaa
Mwanadada kutoka nchini Uganda Cissy Nansera aliweza kutumia masaa zaidi ya 10,000 katika mazoezi ya Yoga na kuwa na uwezo wa kufanya yale anayoyafanya leo, kitu ambacho sio cha kawaida kwa watu wengi hasa watanzania. Ndani ya kipindi cha MID MORNING FRESH kinachoruka kupitia 255 Global Radio Nansera aliweza kutupitisha katika safari ya kuutawala mwili wake baada ya kupata ajali mbaya ya gari ambayo ilimpelekea kukaa kitandani kwa muda.
“Nilianza Yoga mwaka 2015 baada ya kupata ajali mbaya ya gari ambayo ilikaribia kukatisha uhai wangu lakini niliokoklewa na mkanda wa kwenye kiti cha gari, ulinizuia kuchomoka kutoka kwenye kiti. Lakini nilipata tatizo kwasababu kishindo cha ajali kilikuwa kikubwa na mkanda ulinizuia kwa kasi pia hivyo nikapata mshituko kwenye kifua, sikupata majeraha kwa nje ila kifua kilistuka kwa presha na kupelekea maumivu makali, nilihangaika sana, nikalazwa hospitali kwa miezi kadhaa.” Alisema Nansera.
Na kisha kwa bahati nzuri katika kipindi hicho hicho, mwalimu wangu wa Yoga alihamia Kampala na hospitalini walipendekeza nifanye tiba ya mwili (Physical therapy) , Nilitaka kufanya kitu ambacho kingeweza kunitoa katika hali ile na kujihisi tofauti; “Ah, Mungu wangu, ilikuwa ni mbaya sana, nilihitaji msaada” na Yoga ilifanya hivyo. Unaenda zaidi ya uwezo wa mwili wako, Na hivyo ndiyo nilianza Yoga. Na imeokoa maisha yangu kweli, maana nilikata tamaa mwanzo.
Unaona, Hicho ndio ambacho yoga ilifanya maishani mwangu, Kila mtu ana mahusiano binafsi na Yoga, Urafiki wangu na Yoga unaweza usifanane kama urafiki wako na Yoga. Lakini mara tu utakapoanza kujihusisha ndipo utafahamu Yoga inafaida kiasi gani. Sababu sio tu kama mazoezi mengine ya kimwili. Ndio inahusisha mwili lakini pia akili kwa asilimia kubwa. Inaituliza akili yako katika wasiwasi, inasaidia kuondoa msongo wa mawazo, Yoga pia inakusaidia kutulia, kulala vizuri usiku na ukishaanza kupata faida hizi hakuna mtu atakuja akutoe mbali na Yoga. Mara zote utasimama na kusema, Hii ni yangu, nitasimama nayo, na hivyo mimi hufanya.
Mwanzon nilikuwa nikiteseka na wasiwasi, hofu, mngandamizo wa mawazo, sikuwa na utulivu lakini sasa nimeweza kuepuka mambo hayo yote
“Yoga ni mazoezi kwa ajili ya mwili, akili na roho. Yoga ni kitu unachofanya ili kupumzisha akili yako. Yoga ni kitu unachofanya ili kufurahisha roho yako. Yoga pia ni kitu unachofanya ili kuimarisha mwili wako. Kwa hivyo ni zoezi kwa uwepo wako wote. Hiyo ndiyo njia bora naweza kuelezea kwa mtu kuelewa kweli. Najua watu wengi husema; “Unajua ni ya kiroho, watu wanatafakari kila wakati na kufanya mambo haya.” Wanafanya hivyo kwa sababu wanashirikiana na akili zao.” Alisema Nansera
Nansera Aliongeza kwa kusema: “Kufanya Yoga hakukufanyi kwamba usifanye majukumu yako ya kila siku. Acha niseme una jukumu, lazima uende kazini lakini wakati huo huo, lazima uchukue wakati wa kula chakula. Ndivyo ilivyo kwa yoga. Chukua muda na upumzishe akili yako. Ukiendelea kushirikiana na akili yako. Jiburudishe. Na kuimarisha mwili wako.”