Hii ndio kauli ya Drake baada ya kuzomewa na mashabiki kwenye show
Wapenzi wa burudani waliohudhuria katika Tamasha la Camp Flog Gnaw Los Angeles iliyoanzishwa na Tyler, lilizua gumzo Jumapili (10 Novemba) usiku kwani Kila mtu alitaka kumjua msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo atakuwa nani na Wengi walitarajia kumuona Frank Ocean na Jina lake ndio wote walikuwa wanalitaja walitarajia kumuona sana kwamba atatokea.
Lakini cha kushangaza zaidi msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo akatokea Drake kitu ambacho kilionyesha watu kutokufurahishwa na ujio wa Drake kama msanii kinara ‘headliner’ wa tamasha hilo hivyo zilizuka kelele za kumzomea hadi kupelekea kushuka ndani ya jukwaa.
Lakini baada ya tukio hilo Drake amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuzomewa na mashabiki wa tamasha la Camp Flog Gnaw, kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema.
“Mchezo umegeuka, nimesaini mkataba wa miaka 10 kutumbuiza katika tamasha la Camp Flog Gnaw, naombeni radhi watoto tutaonana kila mwaka hadi wote mtakapofikisha miaka 30”