Sambaza

John Legend atajwa kuwa mwanaume mwenye mvuto wa kimahaba zaidi Duniani

Gazeti la People’s siku ya jana jumanne limemtaja muimbaji nguli wa miondoko ya RnB Duniani John Legend kama “Mtu mwenye mvuto wa kimahaba zaidi Kwa mwaka 2019” (Sexiest Man Alive for 2019)

Baada ya kupokea heshima hiyo, John Legend aliliambia gazeti hilo, “Nilifurahiya, ila niliogopa kidogo wakati huo huo kwasababu ya presha kubwa.” Aliendelea kwa kusema, “Kila mtu sasa atakwenda kunichagua na kuangalia kama kweli nina mvuto wa kutosha kwa mimi kubeba wadhifa huu.

Mke wa Legend Chrissy Teigen alisema kuwa siri yake sasa imekuwa wazi, ” “my secret is out. I have fulfilled my dream of having boned @people’s sexiest man alive!! an honor!!!” Alisema hayo kupitia mtandao wa Twitter.

John Legend amechukua nafasi hiyo ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Idriss Elba ambaye alikuwa mwanaume mwenye mvuto wa kimahaba mwaka 2018.

24/7 #Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani | Kutusikiliza au kupakua app ya radio Bonyeza Hapa http://bit.ly/_255GlobalRadio

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey