Tunda’ Betri yangu ilizima, najichaji!
Video queen maarufu Bongo Anna Kimaro ‘Tunda’ ametoa kali ya mwaka kwamba ukimya wake unatokana na betri yake kuzima na sasa anaichaji aweze kusikika tena
Akibonga na za motomoto News, Tunda alisema kuna kipindi lazima watu wakusahau kidogo kisha waanze kukukumbuka tena, hivyo kwa upande wake betri yake ilitumika sana na kuzima chaji, Kwahiyo anaichaji. “Unajua ni lazima ufike wakati betri ichajiwe upya ili kama ni gari au simu ishike kasi mpya kwasababu bila hivyo vitakufa na kuzima kabisa. Hivyo, mimi sio kwamba nimezima moja kwa moja, bali najichaji na hivi karibuni tu mashabiki watanisikia tena.” Alisema Tunda.
Imelda Mtema
Toa Maoni Yako Hapa