Sambaza

‘Ukiwa msanii lazima ujitambue, sio kula bata pekee’ Ommy Dimpoz

Mshindi wa tuzo za Afrimma mwaka 2019, katika kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Ommy Dimpoz, amezumgumzia suala lake la kusafiri mara kwa mara na kudai kuwa huwa haendi kula bata pekee bali ni kutafuta ‘connection’.

Sijaelewa watu wakisema bata wanaamanisha nini ni kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa sisi ni ‘brands’, watu wenye ushawishi nikikufungulia email yangu nitakuonesha mialiko, mingine hadi naikataa ili mienendo yangu iendane na kazi, pia connection zinapatikana na tunazitumia vizuri” amesema Ommy Dimpoz.

Aidha Ommy ameongeza kuwa, “Kitu akifanya Ommy kinageuka kuwa bata kwa mfano juzi tu nimetoka kuchukua tuzo za Afrimma, lakini watu hawajauliza hilo, ukishakuwa brands na ukijitambua mambo mengine yanakuwa ni rahisi sana“.

Pia Ommy Dimpoz amesema kuwa tayari ameshafanya kazi tatu na wasanii wakubwa wa kimataifa na mwisho wa mwezi huu ataenda ku-shoot nao video.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey