Sambaza

‘Nipo bize Wema Sepetu nimempa asilimia 50’ – Kadinda

Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Martin Kadinda, amesema sababu ya kutoonekana kuwa karibu na Wema Sepetu ni kutokana na kuwa bize na biashara zake na kujiepusha kwenye vyombo vya habari tofauti na awali.

Martin Kadinda amesema hayo baada ya kuwepo na taarifa kuwa ule ukaribu wao wa mwanzo umepungua ambapo ameeleza,

“Hayo ni mawazo binafsi ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii nipo na Wema Sepetu, Mimi mwenyewe kwangu nilikuwa naye ni kwamba nimeamua tu kumuweka Wema nyuma sio mbele kama ilivyokuwa kwa sababu mimi nina biashara natakiwa kuifanya na yeye anatakiwa aendeleze maisha yake” amesema Martin Kadinda.

Aidha Martin Kadinda ameendelea kusema “Nimejaribu kutofautisha urafiki na kazi kwa sababu zamani labda nilimpa asilimia 80 ya maisha yangu lakini sasa hivi nimeamua kufanya 50 kwa 50 ila sio kwamba kuna utofauti tupo sawa” ameongeza

Pia akizungumzia suala la Wema Sepetu kutojenga nyumba amesema, hayo ni mambo binafsi ya mtu hakuna aliye na ushahidi kama amejenga au hajajenga, kila mtu anakuwa na mipango au mawazo yake ya kufanya.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey