SANCH AKIKAZA KIDOGO TU, KINA VERA HAWAMPATI!
VERA ni mrembo maarufu runingani, mitandaoni (sosholaiti), video vixen (muuza sura kwenye video za muziki) na mjasiriamali wa Kenya anayetajwa kuwa na utajiri wenye gumzo kutokana na namna alivyoupata na kuna madai mazito kuwa ameupata kwa kudanga! Kibongobongo tunao warembo wa aina hii ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kuwa sosholaiti, kuuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii Bongo Fleva, lakini kimsingi wanashindwa kushindana na warembo wenzao kutoka Afrika Mashariki wakiwemo Vera Sidika.
Tunamkumbuka marehemu Agnes Masogange (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi), lakini wapo kina Sanch, Tunda, Poshy Queen lakini pia usiwasahau Gigy Money na Amber Lulu ambao wamejaribu kurusha karata zao kwenye Bongo Fleva baada ya kuona mambo magumu kwenye upande wa sosholaiti. Suala la msingi hapa ni kujiuliza kwa nini wengi wao hawatoboi kwa maana ya kumiliki mijengo mikali, majumba na miradi mikubwamikubwa?
Kuna mahali wanakwama, hivyo suala la msingi ni kujifunza na kuchukua hatua. Kinachombeba Vera ni mvuto kwa maana ya shepu ambayo anaitumia vizuri kutengeneza hela kwa matangazo ya mabango, kutokea kwenye video za wasanii lakini pia kutokea kwenye shughuli za watu kama alivyoalikwa juzikati katika Baby Shower ya Tanasha hapa Bongo, akalamba mpunga wake wa kutosha. Mbali na hilo, mrembo huyo anaingiza mkwanja kwa kupiga picha za matangazo ya nguo za ndani, mrembo huyo anamiliki saluni za masaji na bidhaa za majani ya chai.
Vera mwenye umri wa miaka 30, anatajwa na mitandao ya nchini Kenya kuwa ana utajiri unaokadiriwa ku? kia Dola za Kimarekani milioni 2.5 (zaidi ya shilingi bilioni 5 za Kibongo). Mbali na kuwa na kiasi hicho cha pesa, pia Vera anatajwa kumiliki magari bei mbaya; kwa kifupi huwa anachafuka kwa madini ya dhahabu na Tanzanite. Kwa mfano; mwaka jana alijinunulia saa aina ya Rolex yenye thamani ya shilingi milioni 2.4 za Kenya (zaidi ya shilingi milioni 50 za Kibongo). Lakini ukirudi kwa Sanch,
kila sifa ya kumzidi Vera kwani ana mvuto wa sura hadi shepu. Kinachokosekana kwake ni kujiongeza tu kibiashara kwa maana ya kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inaweza kumuingizia fedha. Sanch akivaa anapendeza na kama ni mavazi, anatinga yaleyale ya gharama kama ambayo kina Vera wanavaa. Sanch ana kiuno kama ‘nyigu’ ambacho Vera hana.
Ana miguu ya bia ambayo Vera anasubiri, usisahau lile jicho lake kali na ukienda kwenye kalio sasa, analo la haja! Lakini pamoja na sifa zote hizo alizonazo, ishu inabaki kuwa ndogo tu, kwenda nao sawa. Ili wakiweka magari makali naye anaonesha, nyumba anaweka miradi naye anakuwa nayo kama yote.
Najua ameshaanza kupiga shoo za kutokea kwenye matamasha mbalimbali hususan nje ya nchi lakini haitoshi, anatakiwa kuwa na mtandao mpana wa kujitengenezea jina lake lizidi kuwa kubwa hususan nje ya nchi. Aweze kumiliki majumba kama ilivyo kwa Vera lakini pia aweze kuwa na magari ya kifahari kama ilivyo kwa Vera ambaye anayaonesha maisha yake kweli ni ya kistaa na umbo lake ni bidhaa tosha inayomfanya aishi vizuri. Asiishie tu kupiga picha kali na kuposti mtandaoni bali apige picha za bidhaa, awe na menejimenti ambayo itamuongoza kutengeneza jina lake, kusambaza bidhaa zake na kuhakikisha anapata matangazo mbalimbali, umbo lake linambeba na inawezekana kabisa!